Latest Posts

BOBI AMTAKA MUHOOZI ULINGONI “NIKISHINDWA NAACHA SIASA, MUHOOZI AKISHINDWA AACHE ULEVI”,

Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP), Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine, amemuita Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kwa pambano la moja kwa moja la ndondi, akisema yupo tayari kupigana naye muda wowote.

Kupitia mtandao wa X Machi 25, 2025, Bobi Wine amesema iwapo atapanda ulingoni na kupigwa na Jenerali Muhoozi, basi atastaafu siasa. Aidha, akimpiga Jenerali Muhoozi, basi Muhoozi atalazimika kuacha ulevi.

Hii inakuja baada ya Jenerali Muhoozi kuandika kwenye mtandao huo kuwa “kumuua Kabobi (Bobi Wine) ni kazi rahisi, rahisi sana. Amesema anapenda ndondi. Namualika kwenye ndondi.”

Katika kujibu kauli hiyo, Bobi Wine aliandika: “Changamoto imekubaliwa. Kama ukinipiga, nitaacha siasa na kama nikikupiga, utaacha pombe. Sema lini, nitasema wapi.”

Majibizano haya yamezua gumzo kubwa mitandaoni, huku wafuasi wa pande zote wakisubiri kuona iwapo pambano hilo litatokea au ni sehemu ya maneno ya kisiasa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!