Latest Posts

KAMPUNI TAKRIBANI 40 ZA UBELGIJI ZATUA NCHINI KUANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

Wafanyabishara na wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji wamealikwa kuwekeza hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, utalii, madini na kadhalika.

Ukaribisho huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Dkt. Seleman Jaffo alipokuwa akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kufungua kongamano la uwekezaji la Tanzania na Ubelgiji linalofanyika, Jumatatu Novemba 25.2024, Serena Hotel, jijini Dar es Salaam

Dkt. Jaffo amesema kongamano hilo linalenga kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili ambapo wafanyabiashara na wawekezaji karibu 40 wa Ubelgiji wamefika hapa nchini ambapo wanatarajia kukutana na wawakilishi wa makampuni karibu 300 ya Tanzania ambapo kwa pamoja watabadilishana mawazo, kuelezana fursa zilizopo ikizingatiwa kuwa Tanzania ina fursa lukuki katika maeneo mbalimbali

“Tunafahamu sana kwamba jambo hili ni lazima liwe na wenyewe, tunashukuru sana makampuni mbalimbali kutoka Tanzania ambao wamejumuika katika mkutano huu, na kwakweli naweza kusema umekuwa ni mkutano wa kwanza ambao umejaa sana watu, watu wamekuwa na shauku kubwa sana ya kuona ni jinsi gani wanatengeneza urafiki” -Dkt. Jaffo

Amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayo dhamira ya kuona uwekezaji unaimarika zaidi kupitia uwekezaji huku malengo mama yakiwa ni kufikia kilele cha mafanikio ya uchumi wa viwanda

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Jestas Abouk Nyamanga amesema amefika hapa nchini akiwa ameambatana na wawekezaji na wafanyabishara kutoka kwenye makampuni 40 ya Ubelgiji sambamba na viongozi wa taasisi zinazosimamia uwekezaji nchini humo ambapo kwa pamoja wataangalia fursa zilizopo kwenye sekta mbalimbali

“Ubelgiji ni miongoni mwa nchi zinazowekeza sana Tanzania na mpaka sasa uwekezaji wao umefikia karibu dola za Kimarekani milioni 430 na uwekezaji huo umekua sana kwenye sekta za kilimo, logistics, masua ya energy, masuala ya mining, masuala ya Hotels nk, lakini tumekuja pia kuangalia sekta zingine hasa sekta ambazo zinaendelea kukua kwa kasi hapa nchini” -Balozi Nyamanga

Sambamba na hilo, Balozi Nyamanga amesema ujumbe huo wa Ubelgiji unatarajia kufanya ziara kwenye ofisi na taasisi mbalimbali za serikali kama vile Bandari, TANESCO, EPZ sambamba na kutembelea maeneo ya utalii hapa nchini ikiwemo Visiwa vya Zanzibar ili kwenda kujionea namna serikali ilivyotengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji nchini

Daud Liganda yeye ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuhusu kongamano hilo anasema kongamano hilo limeandaliwa na TIC kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Ubalozi wa Ubelgiji nchini Tanzania na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ambapo amesema TIC inatazama kongamano hilo kama sehemu ya neema ya juhudi za kuvutia uwekezaji kutoka nchi mbalimbali

Amesema matarajio ya TIC baada ya mkutano huo uwekezaji kutoka Ubelgiji utaongezeka kwa kuwa kuanzia mwaka 1997 hadi Oktoba 2024 TIC imeandikisha miradi takribani 48, ambayo ametaja kuwa haitoshi hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuamsha makampuni mengi zaidi ya Ubelgi kuwekeza hapa nchini

Naye, Balozi Peter Hyughebaert anayeiwakilisha Ubelgiji hapa nchini amesema pamoja na mambo mengine uwepo wa kongamano hilo unatokana na mazungumzo yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo walipokutana kwenye mkutano wa pamoja kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika (EU-AU Summit) uliofanyika nchini Ubelgiji, ambapo  miongoni mwa masuala waliyoyapa kipaumbele kwenye kikao chao ni kuhusiana na ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!