Latest Posts

KWENYE MAENEO AMBAYO UPINZANI HAWANA WAGOMBEA KURA ZITAPIGWA -CCM NJOMBE

News Njombe.
 
Katibu wa Siasa na Uenezi (CCM) mkoa wa Njombe Josaya Luoga ametoa maelekezo kwa viongozi wa chama hicho kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha wanaeleza mambo yaliyofanywa na serikali kwakuwa uchaguzi wa sasa kwenye maeneo ambayo vyama vya upinzani havitafanikiwa kuweka wagombea bado kura zitapigwa.
 
Luoga ameeleza hayo wilayani Ludewa wakati wa uzinduzi wa ligi ya Jollam Property Cup katika kata ya Madilu yenye lengo pia la kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
“Kuna baadhi ya maeneo vyama rafiki (upinzani) havijapata wagombea, niwaambie ndugu zangu tutapiga kura za ndio na hapana na mgombea akipata kura za ndio chini ya 50% maana yake eneo hilo uchaguzi utarudiwa”, amesema Josaya Luoga.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Jollam Property & Insurance bwana Lawi Mnyanga inayojishughulisha na kazi mbalimbali ikiwemo upimaji wa ardhi pamoja na ujenzi amewataka vijana kupunguza ulevi na badala yake wajikite kwenye michezo ili kuimarisha afya zao.
 
Nao baadhi ya wachezaji wa ligi hiyo wametoa shukrani kwa fursa ya ligi hiyo kwa kuwa wanakwenda kuimarisha afya zao huku pia wakiahidi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika November 27,2024.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!