Latest Posts

MAANA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUIFUNGUA NCHI

Tangu kuingia madarakani Machi 2021, Rais Samia Suluhu Hassan ameelezwa kufungua uchumi wa Tanzania kwa dunia, hatua iliyoimarisha mazingira ya biashara za kimataifa na kuvutia wawekezaji zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu ya Tanzania (Mei 2021 na Oktoba 2024), juhudi hizi zimesababisha ongezeko kubwa la biashara za kimataifa kwa asilimia 84%, huku thamani ya biashara ikiongezeka kutoka USD 17.4 bilioni mwaka 2021 hadi USD 31.4 bilioni kufikia Agosti 2024.

Kwa kipindi hicho, takwimu zinaonesha ongezeko kubwa la mauzo nje ya nchi kutoka USD 8.4 bilioni hadi USD 15 bilioni, wakati uingizaji wa bidhaa umefikia USD 16.4 bilioni kutoka USD 9 bilioni, ikionesha kuwa Tanzania sasa inazalisha na kusafirisha bidhaa nyingi zaidi.

Katika kukua kwa uchumi, deni la nje nalo limeongezeka kwa asilimia 33% na kufikia USD 32.6 bilioni, kutoka USD 24.4 bilioni, ikiwa ni hatua ya kawaida kwa nchi zinazowekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu.

Rais Samia ameweka msukumo mkubwa katika kuvutia uwekezaji wa kimataifa, akiimarisha diplomasia ya uchumi na kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa sehemu ya ushindani wa kibiashara katika soko la kimataifa.

Hatua hizi zimeongeza fursa za kiuchumi kwa Watanzania, na kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, viwanda, na biashara.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaona kuwa hatua hizi ni muhimu katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, jambo linalotarajiwa kuvutia uwekezaji zaidi na kuchochea maendeleo endelevu nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!