Latest Posts

MAANDAMANO KENYA: ODINGA AONYA DHIDI YA MAUAJI YA KIHOLELA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, amelalamikia vikali kauli ya Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, aliyewataka polisi kuwafyatulia risasi raia watakaokaribia vituo vya polisi wakati wa maandamano.

Akizungumza baada ya matukio ya machafuko yaliyojitokeza Juni 25, Odinga amesema, “Mtu yeyote anayehamasisha polisi kuwafyatulia risasi wananchi wa kawaida anastahili kulaaniwa vikali.”

Kauli hiyo imeibua tafsiri kuwa ni ukosoaji wa moja kwa moja kwa utawala wa Rais William Ruto — jambo lisilo la kawaida hasa ikizingatiwa kuwa chama cha Odinga kina wanachama watano katika baraza la mawaziri kupitia muundo wa serikali ya muungano mpana (broad-based government).

Matamshi ya Waziri Murkomen yalikuja baada ya baadhi ya vituo vya polisi kushambuliwa wakati wa maandamano, ambapo alidai kuwa alikuwa akisisitiza mamlaka halali ya polisi kulingana na Kifungu B (1) cha Sheria ya Huduma ya Polisi ya Kitaifa – kinachoruhusu matumizi ya silaha kwa lengo la kujilinda au kuwalinda wengine dhidi ya tishio la kifo au madhara makubwa.

Hata hivyo, wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kuwa kauli hizo zinaweza kuhalalisha matumizi mabaya ya nguvu na kuibua mauaji ya kiholela.

Odinga pia alizungumzia maandamano ya Juni 25 yaliyogubikwa na vurugu, uporaji, na vifo vya raia, akilaani vikali wahalifu waliotumia maandamano hayo kama kisingizio cha kuvunja sheria.

Katika hatua ya kutafuta suluhu, Odinga ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa, akihimiza kuwepo kwa maelewano ya pamoja baina ya wananchi na viongozi ili kujenga msingi wa umoja na maridhiano ya kitaifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!