Latest Posts

MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI YAWEKA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA ‘ZIRO’ KIDATO CHA 4

Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imetumia shilingi milioni 43.5, fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kidato cha nne wanaokaa kambi kutoka katika shule 11 za sekondari za kutwa zilizopo kwenye manispaa hiyo.

Akizungumza Januari 27,2025 mkoani mtwara katika kongamano la elimu lililowakutanisha wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2025 na kuhakikisha manispaa inafuta daraja sifuri kwenye matokeo ya kidato cha nne, Mkurugenzi wa Manispaa Mwalimu Hassan Nyange amesema fedha hizo zimetolewa ili kuwasaidia wazazi au walezi gharama za kambi kwa vijana hao na waweze kupata muda mzuri wa kujisomea.

Kongamano hilo limeandaliwa na manispaa hiyo na kufanyikia kwenye manispaa hiyo, lengo likiwa ni kuwaeleza wanafunzi hao kile ambacho wazazi na walezi, halmashauri, shule na taifa kwa ujumla wanakitegemea kutoka kwao.

Aidha mkurugenzi huyo amesema ataanza kulipa fedha ya motisha shilingi 400,000 kwa mwezi kwa wanafunzi 8 wenye ulemavu wanaosoma Sekondari ya Ufundi Mtwara kwa kumpa shilingi 50,000 kila mmoja pamoja na mkalimani wao  ambaye ni mwanafunzi kwa kumlipa shilingi 300,000 kila mwezi.

Ameongeza kuwa sekondari ya Mtwara Ufundi imeongoza kufaulisha kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza kwa shule za ufundi na kwa mara ya kwanza ikifuta daraja sifuri kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya watu wenye ulemavu mkalimani wa walemavu hao, Benjamin Magigi amemshukuru mkurugenzi kwa kuthamini kile ambacho anakifanya na kuwapa motisha walemavu hao ili wazidi kusoma kwa bidii na kuondokana na ziro.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kuitengeneza kesho iliyo bora kwani ili wachague kesho iliyo bora wanatakiwa kuanza kufaulu mtihani na hapo ndipo watakapoanzia kuyatengeneza maisha yao.

Kongamano hilo la elimu linaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Ufaulu Bila Daraja 0 Inawezekana”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!