Latest Posts

MAREKANI YAPIGA WAHOUTHI YEMEN, VIFO VYAPANDA MPAKA 53

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen imeongezeka hadi 53, ikiwa ni pamoja na watoto watano na wanawake wawili, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya waasi wa Houthi.

Washington ilisema mashambulizi hayo ya anga yaliyofanyika Jumamosi yalikuwa ni “maamuzi yenye nguvu” dhidi ya maeneo yanayolengwa na waasi wa Houthi, ikitaja mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu kama sababu kuu.

Kiongozi wa Houthi, Abdul Malik al-Houthi, amesema wapiganaji wake wataendelea kushambulia meli za Marekani katika Bahari Nyekundu.

Ahmed, baba wa watoto wawili kutoka Sanaa, ameliambia shirika la habari la AFP: “Nimeishi Sanaa kwa miaka 10, nimesikia milio ya risasi katika vita hivi. Lakini sijawahi kuona jambo la kutisha kama hili.”

Waasi wa Houthi wanadai kwamba mashambulizi mapya ya Marekani yamelenga maeneo ya Al Jaouf na Hudaydah mapema Jumatatu. Hata hivyo, Marekani haijatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!