Latest Posts

MJADALA MPANA KUHUSU ‘KOSA LA UBAKAJI NA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI’

 

Hukumu iliyotolewa hivi karibuni na  Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Bukoba, mkoani Kagera iliyosema kufanya mapenzi na mwanafunzi kuwa si kosa kisheria imeibua mjadala na maswali mengi miongoni mwa wadau hapa nchini huku wadau wengi wa masuala ya sheria wakionesha kukubaliana na hukumu hiyo

Baadhi ya wadau hao wa sheria (Wanasheria, Mawakili)  waliozungumza na Azam TV wamekiri kuwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi halipo kisheria isipokuwa neno linalotambulika kisheria ni kubaka

“Sheria ipo vizuri kabisa tatizo ni kwamba nadhani watu wameshindwa kuitafsiri judgement na Mheshimiwa Judge, judgement ilijikita kwa kitu ambacho kulikuwa mbele yake, kilichokuwa mbele yake ni kwamba mtu amehukumiwa na kufungwa jela kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wa shule (prohibited sexual intercourse), hicho kifungu hakiko kwenye sheria zetu zozote, lakini kufanya mapenzi na mwanafunzi ni kosa kwa kuwa utakuwa umefanya ubakaji ikiwa mtoto huyo yuko chini ya miaka 18” -Wakili Makore

Wakili Ferdinand Makore ameendelea kufafanua kuwa endapo mtendwa ambaye ni mwanafunzi atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 18 basi mtuhumiwa anaweza kushtakiwa kwa kosa la kumpa mimba au kumuoa mwanafunzi, kwa mujibu wa sheria ya elimu, kifungu cha 60(A), hivyo hakuna mwanya wowote ambao umeachwa kwenye sheria isipokuwa mjadala umekuja kufuatia hukumu iliyokuwa imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya na namna Hakimu aliyekuwa amesikiliza kesi hiyo alivyotafsiri kifungu hicho cha sheria

“Tatizo lilikuwa ni tafsiri tu, kwa sababu kosa la kufanya mapenzi lipo lakini haliitwi hivyo, ishu ni kwamba jinsi lilivyokuwa limeitwa, linaitwa ubakaji, sasa ubakaji uko limited kwa mtoto ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18, kwa hiyo  ukifanya mapenzi na mwanafunzi ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18 maana yake umefanya mapenzi kwa jina la ubakaji, kwa hiyo ambacho kiliandikwa kule ni kufanya mapenzi kumbe ilipaswa kuandikwa kufanya ubakaji” -Wakili Makore

Ikumbukwe kuwa, Mwezi Oktoba mwaka huu (2024) Jaji Gabriel Malata wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Bukoba, mkoani Kagera ndiye aliyetoa hukumu hiyo baada ya aliyekuwa mshtakiwa wa shauri hilo Thadeo Pastory kuhukumiwa na Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Misenyi kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi na ndipo alipoenda kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba na hatimaye rufaa yake akashinda

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!