News, Njombe.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Dkt. Scholastika Kevela ametaka walimu hususani wanaofundisha watoto wenye ulemavu kupewa heshima kubwa kutokana na hali wanayokutana wakati wa kuwabadilisha watoto wenye changamoto za ulemavu.
Mwenyekiti ameeleza hayo alipowatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule ya awali na msingi Idofi iliyopo kata ya Mlowa, Halmashauri ya Mji wa Makambako wilayani Njombe.
Ambapo licha ya kuwatembelea na kutoa faraja kwa walimu ameweza kukabidhi Televisheni (TV), ndoo za kuhifadhia maji na vifaa vya kufanyia usafi kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo.