Latest Posts

NANYAMBA WAPITISHA BAJETI YA MAKADIRIO YA SHILINGI BILIONI 24 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Kutokana na kutokuwepo kwa shule ya sekondari katika kata ya Kianga, Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo limetenga kiasi cha Shilingi milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari kwenye kata hiyo.

Hayo ameyazungumza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Mshamu Munde kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya makadirio ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Hata hivyo kikao hicho kimepitisha shilingi bilioni 24 kwaajili ya kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule katika kata ya Kianga.

“Kata hiyo ni kata pekee isiyokuwa na shule ya sekondari hivyo tumeona ni vyema kiasi hiki cha fedha kitengwe kwaajili ya ujenzi wa shule hii.” Amesema Munde.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hamisi Maliki amesema kwa umoja wao wamekubaliana kupitisha kiasi cha shilingi bilioni 24.4 kwenye baraza hilo kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri yao kwa kukarabati miundombinu mbalimbali chakavu kwenye maeneo ya barabara, maji, umeme na vituo vya afya.

“Kupitia bajeti hii tutahakikisha tunaenda kutatua changamoto nyingi zinazotukabili ndani ya halmashauri ambazo zinapelekea kukwamisha maendeleo”, ameeleza Maliki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!