Latest Posts

RIPOTINI HABARI KUHUSU MIENENDO YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA : JAJI (MST.) MWANGESI

Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi amevihimiza vyombo vya habari nchini kuandika habari za kichunguzi  zinazohusu mienendo ya viongozi wa umma ili kuwabaini viongozi wasio na maadili ya utumishi wa umma na kuchukuliwa hatua stahiki.

Jaji Mwangesi ametoa rai hiyo akizungumza katika kikao cha Sekretarieti ya maadili na Wahariri wa Vyombo vya bahari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 30, 2025 ambapo amesema kalamu za wahiriri zina nguvu kubwa kukuza maadili ya viongozi wa umma kwa kuchochea uadilifu na uwajibikaji  kwa Viongozi wa Umma.

Ameongeza kuwa vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika kuibua taarifa fiche  zinazoisaidia jamii kujua hali ya uadilifu wa viongozi nchini.

Aidha, kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani, Jaji Mwangesi amewaasa wahariri na waandishi wa habari kuzingatia weledi wa taaluma zao kwa kutoa taarifa stahiki zenye ulinganifu  zinatakazo wasaidia wananchi kuchagua viongozi wenye uadilifu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!