Latest Posts

TARIME YAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU KWA KUDUMISHA MICHEZO

Na Fredrizzo Samson
Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Halmashauri ya Mji wa Tarime imeandaa bonanza la michezo mbalimbali kwa kushirikisha watumishi pamoja wanamichezo kutoka Tarime Vijijini na mpakani mwa nchi jirani ya Kenya.
Bonanza hilo la michezo limejuisha michezo kama vile mpira wa miguu, mchezo wa wavu (netball), mchezo wa kikapu (basketball), kukimbia na magunia, kuvuta kamba sambamba na mchezo wa kufukuza kuku ulioibua hisia za furaha kwa wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu kilichopo Tarime mjini.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele ambaye amewakilishwa na Katibu Tawala wa Halmashauri mji wa Tarime, Mwl. Saul Mwaisenye,
Akitoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa michezo hiyo, Katibu Tawala wa halmashauri hiyo, Mwl. Saul Mwaisenye amewaasa wananchi kuendelea kudumisha amani na kuendeleza michezo kwani michezo ni afya na ajira.
Aidha, maadhimisho hayo yamehitimishwa  kwa zoezi la upandaji miti katika shule ya Gicheli Secondary iliyopo kata ya Nkende, Tarime mjini.
Tembelea Channel ya Jambo Tv kwa urefu wa habari hii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!