Latest Posts

UONGOZI WA KIMKAKATI KUTOKOMEZA VIFO VYA AKINAMA NA WATOTO, MAKAME

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amewaasa wataalamu wa sekta ya afya Mkoa wa Morogoro kuendelea kutoa uongozi bora katika vituo vyao vya kutolea huduma za afya ili kufikia malengo ya kukabiliana na changamoto za kukabiliana na vifo vya akimama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.

Aidha, amewapongeza wataalamu wote wa afya Mkoa wa Morogoro kwa kazi nzuri wanayoifanya kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za Mama na mtoto hali iliyopelekea Rais kutambulika na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation ya nchini Marekani na kumtunuku Tuzo Maalumu ya The Global Goalkeepers Awards kutokana na uongozi bora katika kukabiliana na vifo vya akina mama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.

DC Makame ameyasema hayo katika kikao cha wataalamu wa Sekta ya Afya Mkoa wa Morogoro kilichofanyika wilayani Gairo, waliokutana kufanya tathmini ya utendaji kazi na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za Mama na mtoto Mkoa wa Morogoro, ambapo amesisitiza kuwa uongozi ndio msingi wa  maendeleo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!