Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ambapo tarehe 20 Julai 2024 ndio siku ya uandikishaji na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kupata haki zao za msingi .
Akizungumza Julai 17, 2024 katika vijiji vitano vya Mkoa wa Kigoma, mwenyekiti Chatanda amesema viongozi wa UWT wapo katika mkoa huo katika kuhamasisha wananchi Kwenda kujiandikisha ili kupata haki yako ya msingi .
Mwenyekiti Chatanda amesema, ni jukumu lao kama viongozi kuhakikisha hamasa inakuwa endelevu kwa kuwa uandikishaji huo ni wa wiki mbili hivyo amewataka kila mwananchi kwenda site kama viongozi wenu kwa kuwa sasa ni wakati kwenda kuhamasisha.
“UWT tupo hapa Kigoma mpaka daftari litapozinduliwa na tutaendelea na ziara ya mikoa ya mwanzo wa daftari ili kuendelea kuhamasisha daftari la mpiga kura ili mwananchi aandikishwe na apate haki yake ya msingi hivyo niwaombe wananchi wa Kigoma kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura“ alisema Chatanda