Kocha mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea Derby ya Kariakoo ameitaka klabu ya Simba kuingia uwanjani na kucheza mpira na sio kwa lengo la kulipa kisasi. “Mchezo wa kesho ni mchezo mgumu na tunajua wanataka kuja kucheza ili washinde mechi na kulipa kisasi lakini tumejiandaa kwa hilo, sisi tuna timu imara ambayo inaweza kucheza kwenye presha ya aina yoyote, kama wanadhani wakija na presha ya kulipa kisasi inaweza kuwasaidia basi linaweza kuwa kosa ” Gamondi . Mchezo namba 180 wa ligi kuu ya NBC utapigwa kesho kati ya watani wa jadi Simba na Yanga katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga SC watakuwa ndio wenyeji wa mchezo huo.