Latest Posts

WACHIMBAJI WADOGO GEITA KUANDAA KONGAMANO KUBWA KUMPONGEZA RAIS SAMIA

Chama cha Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Geita (GEREMA) kimeandaa kongamano kubwa litakalofanyika Mei 11, mwaka huu katika mji mdogo wa Katoro, kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya madini, hususan kwa wachimbaji wadogo.

Kongamano hilo litaambatana na shughuli mbalimbali za kijamii na burudani, ikiwa ni pamoja na mashindano ya ulaji wa nyama na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa GEREMA, Bw. Taitus Kabuo, amesema maandalizi ya tukio hilo yamekamilika kwa asilimia 100 na tayari wameanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Tunaamini tukio hili litakutanisha wachimbaji kutoka maeneo tofauti, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya madini. Tunatarajia kuwa na wageni wengi watakaoshiriki kwa namna mbalimbali katika kongamano hili,” amesema Kabuo.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, pamoja na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), Bw. John Bina.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!