Latest Posts

WAFANYABIASHARA MTWARA WAHIMIZWA KUWASILISHA KERO ZAO KWENYE MABARAZA YA BIASHARA

Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika sekta mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kufanya shughuli hizo.

Akizungumza Novemba 21,2024 mkoani Mtwara wakati wa kikao cha 8 cha baraza la biashara la mkoa wa Mtwara mwaka 2024, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema lengo kubwa la kuanzisha mabaraza hayo ya biashara hususani ngazi za wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi ya kuwakutanisha viongozi wa serikali na sekta binafsi katika kila ngazi ya utawala.

Pia kujadiliana namna ya kuboresha biashara na uwekezaji kwa ajili kukuza sekta binafsi ambayo ndiyo muhimili muhimu katika kukuza uchumi wa maeneo yao na taifa kwa ujumla.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwasihi sekta hizo binafsi kutokana na mazingira hayo, kuendelea kuwa na utamaduni wa kuwasilisha kwenye mabaraza ya biashara kero na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye biashara kwa ajili ya majadiliano na kuzipatia ufumbuzi.

”Tunapokuwa na mabaraza haya ya biashara yanayokutana na utaratibu huu endelevu tunakuwa na uwezo wa kuondoa kero na changamoto ninyi wenzetu mnazokutana nazo kwenye maeneo mbalimbali ili kuyapatia ufumbuzi kwa wakati.” Amesema Sawala

Halikadhalika ametoa wito kwa viongozi wote mkoani humo, kutumia mabaraza hayo kupokea na kushughulikia kero za wafanyabiashara wao ambapo katika kikao hicho baadhi ya ajenda zilizojadiliwa ikiwemo mpango wa dhamana ya mkopo itakayokuwa chachu kwa biashara katika kutambua fursa ya dhamana ya mikopo.

Hata matumizi ya chumvi yenye madini joto ambayo ni miongoni mwa kero kubwa katika utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe mkoani humo, licha ya juhudi mbalimbali zinazofanyika za kuhamasisha wafanyabiashara kupunguza chumvi yenye madini joto kwa faida ya jamii lakini pia uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadogo.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyabiashara mkoani humo, Emmanuel Mwambe ameipongeza serikali kwa yale yote yanayofanyika hasa kutambua mchango wa wafanyabiashara katika maendeleo chanya nchini na ni matumaini yao kuwa jitihada hizo zitakuwa endelevu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!