Latest Posts

WAZIRI NDUMBARO AKUTANA NA RC MAKONDA, KUONGEZA ARI KAMPENI YA MAMA SAMIA ARUSHA

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Machi 03, 2025, amekutana na kuzungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro Ofisini kwake Jijini Arusha, ambapo Waziri Ndumbaro amefika Mkoani Arusha kukagua utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, Kampeni ambayo imezinduliwa Machi, Mosi ikiambatanishwa na Wiki ya wanawake ambayo kilele chake kinafanyika Machi 08, 2025, Mgeni rasmi akiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kampeni ya Mama Samia kwa Mkoa wa Arusha inafanyika kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Makonda akitoa wito kwa wananchi wote wa Arusha wenye changamoto mbalimbali za kisheria kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo iliyoasisiwa na kufadhiliwa na Rais Samia katika jitihada zake za kupunguza migogoro ya kijamii kote nchini na kutoa msaada wa kisheria na Mawakili kwa wasiokuwa na uwezo na wale wa pembezoni wasiofikiwa kwa karibu na huduma za sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!