Zaidi ya Shilingi 30,000,000, kombe pamoja na zawadi mbalimbali zitakabidhiwa kwa washindi wa Matiko Cup Machi 2, 2025 ni baada ya Februari 28, 2025 kuibuka washindi katika fainali ambapo Nyamisangura FC iliibuka mshindi wa kwanza na kupata 15,000,000, mshindi wa pili Giant ilipata 10,000,000, mshindi namba tatu watumishi ilipata 5,000,000 na mshindi wa nne alipata 2,000,000.
Ushindi wa Nyamisangura dhidi ya Giant ulitokana na magoli 3 ya penati baada ya kipindi cha dakika 90 wote kutoka bila goli, Giant walifunga goli 1 na kukosa penati 3 watumishi dhidi ya Tarime united magoli 2 kwa goli kwa goli 1.
Matiko Cup ilizinduliwa januari 3,2025 mashindano ya timu 20 yakaanza timu 1 ilikuwa ya Tarime vijijini na 19 zilikuwa za Tarime Mjini ikiwemo ya watumishi wa Halmashauri ya Mji Tarime mashindano yamefanyika zaidi ya mwezi mmoja na hatimaye Nyamisangura fc kuibuka mshindi na kujitwalia kombe na shilingi 15,000,000.
MKurugenzi wa Matiko Cup ambaye ni Mbunge Viti maalum Esther Matiko amesema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na Madini, Dotto Biteko atakuwepo Tarime uwanja wa shamba la bibi Machi 2, 2025 kwaajili ya kuwakabidhi zawadi washindi na kuongeza kuwa atakuwepo pia msanii Harmonize pamoja na nyama choma festival hivyo watu watakesha uwanjani hapo.
“Niwapongeze Tarime united, niwapongeze Hamza, niwapongeze wenzetu wa Giant, lakini pia nipongeze timu zote zilizoshiriki nusu fainali,nashukuru timu zote 20 zilizoshiriki zote ni bora lakini lazima mshindi apatikane niwapobgeze nyamisangura ambao wanaenda kuchukua kombe timu shirikishi nazo kwa kutambua ushiriki wake tutawapa tuzo na shilingi 500,000 kila timu kwaajili ya kuanzia Manisha” alisema Matiko
Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Samweli Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara mstaafu alimpongeza Esther Matiko kwa kutobagua vyama vya siasa katika michezo huku akiahidi kushirikiana naye .
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha michezo, utamaduni na sanaa Halmashauri ya Tarime Mji Teddy .E.Musyangi alimshukuru Matiko Kwa kuiheshimisha Tarime kupitia na michezo pamoja na kuwashukuru Mashabiki kuwa watulivu pamoja na nidhamu uwanjani.
Nahodha (Captain) wa timu ya Nyamisagura Fc Nashon Majeneza alisema chanzo cha ushindi wao ni mwalimu wao aliyewafundisha na kuwaandaa vizuri hadi kufikia hatua ya kupata ushindi huo ulimpatia furaha kubwa.
Kocha wa Nyamisangura Fc Amos Joseph amewaomba viongozi wengine kuiga mfano wa Matiko ili kuwasaidia vijana kuondokana na changamoto mbali mbali kama vile ulevi hivyo kwa kuanzisha michezo itapunguza changamoto kwa vijana.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Tarime na ambaye ni Diwani wa kata ya Nyamisangura iliyochukua ushindi Thobias Elias Ghati kwa upande wake alimpongeza Matiko Kwa ligi hiyo na kufurahi timu hiyo kuchukua ushindi wa milioni 15,000,000.
” Timu zialianza nyingi kwenye mtaa wangu nilikuwa na timu mbili Tarime united na Nyamisangura wote ni vijana wangu nianze kwa kuwapongeza Giant, nianze kuwapongeza na watumishi hiyo ni timu yangu ya Halmashauri lakini zaidi niipongeze timu yangu ya Nyamisangura hapa tulipo tumeondoka na ushindi wa milioni 15 alizozitoa Mhe Heshimiwa Esther tunaondoka nazo hapo vipi? ” Alisema Ghati