Kada wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi aliedumu katika ngazi ya Udiwani kwa miaka 31 amestaafu rasmi na kubainisha kuwa ni vyema kuwa na kiasi katika kutumikia wananchi ili wasikichoke.
Akizungumza na Jambo TV William Mbogo ambaye katika uongozi wake alihudumi ngazi ya Meya wa Manispaa ya Mpanda mwaka 2025-2020 amesema katika kipindi chote jambo ambalo lilimpa ugumua ni suala la ununuzi wa gari la taka lililogharimu Tsh.milioni 92 ambapo katika manunuzi yake kulikuwa na sintofahamu ya matumiizi ya fedha.
Amebainisha kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kutoa nafasi Kwa watu wengine waweze kuhudumia wananchi wa kata hiyo ya Majengo iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambapo ambapo pia ameshauri wanasiasa kutochukua muda mrefu kwenye nafasi ya uongozi kwani wananchi wanaweza kukuchoka.
Diwani huyo amehudumu Kwa miaka 31 ya uongozi ambapo tangu uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi uliunganishwa na serikali za mitaa ambapo walihudumu kwa miaka 6 kutoka mwaka 1994 hadi mwaka 2000.
Video nzima ya mahojiano haya inapatikana katika you tube ya Jambo online tv.