Latest Posts

MARA YA PILI: HERSI SAID AONDOLEWA MCHUJO WA CCM KONGWA

Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said, ameshindwa kupenya kwenye mchujo wa majina 13 ya wagombea ubunge Jimbo la Kongwa, ikiwa ni mara ya pili jina lake kuondolewa katika mchakato wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwananchi, Hersi ameungana na wagombea wengine 11 waliokatwa katika mchujo huo, huku aliyeshika nafasi ya pili kwenye kura za maoni za Agosti 4, 2025, Isaya Mngurumi, akifanikiwa kupenya. Mapema leo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, alithibitisha kuwa Hersi alikuwa miongoni mwa makada 24 waliojitokeza kuwania ubunge wa jimbo hilo.

“Ni kweli Hersi ni miongozi mwa watiania wa nafasi ya ubunge ndani ya chama chetu, subirini taratibu zingine tutawajulisha, bado tunasubiri majina tuanze kampeni,” alisema Mkaugala kabla ya matokeo ya mchujo kutangazwa.

Hata hivyo, jina la Hersi halikuwemo kwenye orodha iliyotolewa baadaye, sambamba na jina la Mwalimu Deus Seif, aliyeshika nafasi ya tatu kwenye kura za maoni.

Hii ni mara ya pili Hersi kukatwa katika mchakato wa CCM mwaka huu, baada ya awali kushindwa katika Jimbo la Kigamboni ambapo jina lake halikujumuishwa kwenye walioteuliwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!