Shauri la kikatiba na 7300/2026 lililofunguliwa na Nashon Nkung na wenzake limesikilizwa kwa maswali ya Dodoso ambapo upande wa wajibu maombi ukianza na Tundu Lissu(mjibu maombi wa tatu) aliuliza maswali ya dodoso kwa mashahidi.
Shahidi wa kwanza alikuwa Wakili Kulwa Maduhu ambaye pia ni Mleta maombi wa tatu katika kesi hii wakilalamikia juu ya mawakili wa Lissu kuzuiwa kumuona mteja wao aliye katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kutokana na mashtaka ya uhaini yanayomkabili.
Kikao cha Shauri hilo la Kikatiba kinaketi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya jopo la Majaji watatu (3) ambao ni Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Evaristo Longopa limeahirishwa mpaka kesho Julai 21, 2026 ambapo baada ya maswali ya dodoso kutoka kwa Lissu, Upande wa wajibu maombi na upande wa waleta maombi shauri litaendelea kesho kwa mashahidi wengine kuhojiwa maswali ya dodoso.
Katika maswali hayo Lissu akirejea nyaraka mbali mbali za kumbukumbu ikiwemo kitabu cha kumbukumbu ya wageni wanaoingia Geereza ya Ukonga kwa nyakati tofauti tofauti Wakili Nashon Nkung, Paul Kisabo na Kulwa William Maduhu wamekuwa wakiingia gerezani na kujisajili wakijitambulisha kuwa wao ni mawakili wake.
Alimhoji maduhu kama ni sahihi kuwa Oktoba 28, 2025 Wakili Maduhu na Kisabo walianza kukutana na kadhia ya kuzuiwa kuingia magereza kwa kile walichoelezwa kuwa wao si sehemu ya mawakili ambao wapo kwenye orodha ya kumtembelea Lissu jambo ambalo Maduhu alikiri ni kweli.
Katika maswali ya dodoso Maduhu aliendelea kukiro kuwa ni zaidi ya mara moj alikuwa akizuiliwa na baadae alipoulizwa kama kuwa Albino ni sababu ya yeye kuzuia akasema ni kweli.
Lissu: Hiyo Tarehe 28, Oktoba 2025 ulikwenda Ukonga ukiwa na wakili mwenzako Gaston Shundo Garubindi
Maduhu: Kweli
Lissu: Akitakiwa kuangalia kama Wakili Garubindi yupo katika orodha na kueleza
Maduhu: Ni miongoni mwa mawakili kumi walioruhusiwa.
Lissu: Siku hiyo maoni ya Afisa Msimamizi wa Ukonga(OC) alisema aruhusiwe mwenye kibali katika orodha ya mawakili wa mahabusu huyo lakini Kulwa Maduhu hayupo kwenye orodha hiyo ukaambiwa toka hapa
Maduhu: Ni kweli
Lissu alimtaka Maduhu kuangalia aangalie kama kwenye orodha kun wakili mwingine aliyeandikiwa maoni sawa na hayo ambapo alijibu hakuna.
Alimtaka pia aieleze Mahakama kama mfungwa anaetaka kutembelewa na mawakili anapaswa kuorodhesha majina jambo ambalo shahidi alijibu kwa uelewa wake sio sahihi.
Lissu alimhoji kama kuna lolote alilomkosea Bwana Jela wa Gereza la Ukonga Akaeleza kuwa halipo kwani alishaigia mara tatu bila shida.
Baada ya hapo Lissu alimuomba radhi maduhu akisema kuwa kuna swali hapendi kuliuliza lakini alilazimika swali hilo alimhoji akisema “wewe una tatizo la ngozi(albinism) ni kweli au si kwei kwamba nchi hii kumekuwa na vitendo vya kuwabagua na kuwadhalilisha wenye hali kama yako:
Maduhu: Ni kweli na kuwa vitendo hivyo ni vya ubaguzi na kuwa mimi peke yamgu nimekuwa nikibaguliwa nlibaguliwa kwa sababu ya hali yangu
Lissu alimuuliza maduhu kuwa yeye pamoja na Kisabo na walituma ujumbe baada ya kuzuiliwa kisha akaandika orodha ya kumuongeza Maduhu na Kisabo. Akidadavua kuwa baada ya hapo Kisabo aliruhusiwa kuanza kumuona Lissu huku Maduhu akizuiliwa.
Maduhu alituma ujumbe Lissu akamuongeza Maduhu, Dickson Matata Deogratius Mahinyila na wengine na kueleza kuwa amekuwa akitembelewa na mawakili wengine ambao hawapo hata kwenye orodha huku akiibua hoja kuwa kuna ubaguzi kati ya mawakili binafsi na mawakili wa serikali kuwa mawakili wa serikali ZCO, DCEA hawakaguliwi hawapekuliwi na wala hawasimamiwi.
Baada ya Lissu kumaliza maswali yake wakili wa mleta maombi wa kwanza mpaka wa tatu ambaye ni Wakili wa Serikali Mwandamizi Stanley alihoji maswali akitaka kupata ufafanuzi kwa maduhu kama kwenye kiapo na hati ya madai.
Wakili: Kwenye hati ya madai na kiapo uliweka taarifaza kikosi kazi cha UN
Maduhu: sikuweka
Wakili: Kuna sehemu ulilalamika mbele ya jaji Mkwizu
Maduhu: ndio
Wakili: Kwenye kiapo chako na ushahidi wako kuna sehemu umeandika kuwa unabaguliwa kwa rangi yako
Maduhu: Hakuna sehemu niliyoandika
Wakili: Kuna sehemu mkuu wa magereza alisema sikiliza maongezi yao
Maduhu:(alikuwa akionyesha huku wakibishana na baadae majaji wakasema watakagua nyaraka na kuamua)
Baada ya hapo Wakili Edson Kilatu ambaye ni wakili wa waleta maombi alihoji maswali ya dodoso
Wakili: Alipotakiwa kufafanua juu ya kufuata utaratibu kabla ya kwenda mahakamani hebu tueleze
Maudhu: Nimeomba mara kadhaa kuonana na Mkuu wa Gereza zaidi ya mara mbili na sikufanikiwa
Wakili: Kwa nini ulijibu kuwa ubaguzi umetokana na Albinism
Maduhu: Nimeshiriki kufanya kampeni inashangaza kuna ubaguzi huu hasa kutoka kwa uongozi wa magereza wa sasa unanitendea ubaguzi.
Shauri litaendelea kesho…