Latest Posts

TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA 26 YA NGUVU KAZI/JUA KALI KIGALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus C. Sangu, ametangaza kuwa Tanzania itashiriki Maonesho ya 26 ya Wajasiriamali Wadogowadogo, Wadogo na wa Kati (MSMEs) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, maarufu kama Nguvu Kazi/Jua Kali, yatakayofanyika jijini Kigali, Rwanda, kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 8, 2026.

‎Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maonesho hayo yatawakutanisha wajasiriamali takribani 1,000 kutoka nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwakilishwa na wajasiriamali 250.

‎Maonesho ya mwaka huu yataongozwa na kaulimbiu isemayo, “Kuendeleza Mnyororo wa Thamani kwenye Sekta ya Ngozi na Kilimo cha Bustani (Matunda na Mbogamboga) katika Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

‎Waziri Sangu amesema maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wajasiriamali kurasimisha shughuli zao kwa kuwapatia fursa ya kutangaza bidhaa, kubadilishana taarifa na uzoefu, kukuza ujuzi, kupanua masoko ya bidhaa pamoja na teknolojia za uzalishaji. Aidha, maonesho hayo yanatarajiwa kuchangia kuongeza fursa za ajira zenye staha kwa Watanzania.

‎Wajasiriamali wanaotaka kushiriki wametakiwa kujisajili kuanzia Julai 23 hadi Septemba 30, 2026 kupitia fomu rasmi ya usajili iliyotolewa na waandaaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!