Latest Posts

BOTI 2 MPYA ZA DORIA ZAZINDULIWA KUONGEZA ULINZI BAHARINI NA MAZIWA MAKUU

HABARI PICHA:

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo tarehe 31 Julai, 2026, amezindua boti mbili mpya na za kisasa za doria katika viwanja vya Bandari ya Dar es Salaam. Boti hizo, zilizopewa majina ya PB Sailfish 02 na PB Sailfish 03, zinaongeza nguvu katika ulinzi wa rasilimali na mipaka ya bahari pamoja na maziwa makuu, zikifuatia uzinduzi wa boti ya kwanza (PB Sailfish) uliofanyika Machi 2, 2024.

Boti hizi zimejengwa nchini Japan kwa teknolojia ya hali ya juu inayozikubali kufanya kazi katika mazingira magumu ya baharini. Sifa zake kuu ni pamoja na mwendokasi wenye kufikia kasi ya zaidi ya noti 52 (takribani kilomita 96.3 kwa saa), jambo linalozifanya kuwa miongoni mwa boti za kisasa zenye mwendo wa kasi zaidi duniani. Kasi hii inaziwezesha kutumia takribani dakika 30 tu kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar. Aidha, kila boti ina uwezo wa kubeba hadi watu 12 kwa wakati mmoja na zimefungwa mifumo ya kisasa ya urambazaji (navigation systems), mawasiliano ya haraka, na vifaa vya uokoaji vinavyokidhi viwango vya kimataifa vya usalama.

Mradi huu umetekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 2 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5) ukiwa ni ufadhili kutoka kwa Serikali ya watu wa Japan kupitia UNDP. Mradi huu uliodumu kwa mwaka mmoja tangu Machi 2025, haukuishia kwenye ununuzi wa boti pekee, bali ulihusisha pia mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la mwani na ujenzi wa kikaushio cha mwani na usimikaji wa mashine za kusagisha mwani katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Uzinduzi huu umetajwa kuwa hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uwezo wa kufanya doria, ufuatiliaji, na uokoaji wa haraka katika maeneo yake ya maji, huku ikisaidia kukuza uchumi wa buluu kupitia zao la mwani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!