Latest Posts

CHINA YAWAPA WAZAZI RUZUKU YA MAELFU KWA KILA MTOTO ILI KUKUZA IDADI YA WATU

Serikali ya China imeanza kutoa ruzuku ya takriban Shilingi 1,314,000 kwa mwaka kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitatu, ikiwa ni hatua mpya ya kitaifa inayolenga kuhamasisha ongezeko la viwango vya uzazi vinavyoendelea kushuka nchini humo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, mpango huo unatarajiwa kusaidia takribani familia milioni 20 kwa kugharamia sehemu ya mahitaji ya kulea watoto wadogo, huku taifa hilo likikabiliwa na changamoto ya kupungua kwa idadi ya watu.

Kiasi hicho ni sawa na yuan 3,600 kwa mwaka kwa kila mtoto — sawa na dola za Marekani 500 au pauni 375 za Uingereza — na kitaanza kutolewa kwa awamu kuanzia mapema mwaka huu wa 2025.

Aidha, wazazi wanatarajiwa kupokea hadi yuan 10,800 kwa kila mtoto ndani ya kipindi chote cha miaka mitatu ya kwanza, ambacho ni sawa na takriban Shilingi 3,942,000 za Kitanzania.

Mpango huu ni hatua ya kitaifa ya kwanza kabisa ya aina yake, japo baadhi ya mikoa nchini humo ilishaanza majaribio ya ruzuku kama njia ya kukabiliana na gharama kubwa za maisha ambazo zimechangia wazazi wengi kuahirisha au kutoamua kupata watoto.

Familia zilizo na watoto waliozaliwa kati ya mwaka 2022 hadi 2024 pia zitaruhusiwa kutuma maombi ya kupata ruzuku hiyo kwa masharti maalum.

Hatua hii inaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa China wa kupambana na athari za sera ya zamani ya mtoto mmoja iliyodumu kwa miongo kadhaa kabla ya kufutwa rasmi mwaka 2015.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!