Latest Posts

HOSPITALI YA RUFAA TEMEKE YAPOKEA MAGARI MAWILI YA KUBEBEA WAGONJWA

Hospitali ya rufaa ya Temeke, Dar es Salaam (TRRH) imepokea rasmi magari mawili ya kubeba wagonjwa ambayo yamezinduliwa na Dorothy Kilave ambaye ni Mbunge wa jimbo la Temeke, imeelezwa ujio wa magari hayo unaenda kuboresha huduma za rufaa na za dharura zilizopo Hospitalini hapo, na kufanya idadi ya magari ya kubeba wagonjwa kufikia matano

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Kimaro amethibitisha maboresho hayo wakati akiwasilisha taarifa fupi ya utendaji kazi na maboresho katika hafla ya ugawaji wa magari ya kubeba wagonjwa mbele ya mgeni rasmi Mbunge Dorothy Kilave

Dkt. Kimaro ameeleza mafanikio mbalimbali ya Hospitali hiyo moja ikiwa ni kununua kifaa tiba kinachoitwa laparoscopy tower ambacho kitawezesha Hospitali kufanya upasuaji kwa njia ya tundu ndogo, hivyo kupunguza rufaa ya wagonjwa kwenda katika Hospitali za juu, aidha kupitia utendaji mzuri wa timu ya uendeshaji wa huduma za afya, Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma za usafishaji damu (dialysis), na ndani ya wiki kadhaa imefanya sesheni 28 kwa wagonjwa nane waliopatiwa huduma

Kwa upande wake, Mbunge Dorothy Kilave amepongeza juhudi za Hospitali hiyo katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, amesema kuwa kila anapofika Hospitalini hapo anakuta kuna maboresho mapya ambayo wananchi wa Temeke wamekuwa wakiyatamani

Kilave ametoa shukrani na pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia na kusikiliza mahitaji ya majimbo mengi

Pia, ameuhakikishia uongozi wa Hospitali hiyo juu ya uwepo wa fedha zitakazowezesha ujenzi wa ghorofa sita litakalosaidia kupunguza na kuondoa changamoto ya ufinyu wa eneo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!