Latest Posts

MTOTO AFARIKI, WAWILI WAJERUHIWA AJALI YA GARI MWANZA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara na mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, Emmanuel Ntobi (41) kwa kosa la kusababisha ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha mtoto mmoja na kujeruhi watu wengine wawili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa imesema ajali hiyo imetokea leo Septemba 15, 2026 saa 6:20 katika barabara ya Makongoro eneo la Nyamanoro wilayani ya Ilemela.

“Gari lenye namba za usajili T750 BPH, aina ya Toyota Mark II iliyokuwa ikiendeshwa na Emmanuel Julius Ntobi ikitokea Kona ya Bwiru kuelekea Pasiansi iliwagonga watembea kwa miguu watatu waliokuwa wakivuka barabara kutoka upande wa kulia kwenda kushoto,”.

Aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ni, Johnson Florence (7) mwanafunzi wa darasa la kwanza, Shule ya Msingi Ibungiro huku majeruhi wakiwa ni, Kodo Joel (30) mkulima na mkazi wa Pasiansi, pamoja na Janeth Nambile (3) mwanafunzi wa
chekechea, Shule ya Msingi Pasiansi wote wakiwa wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Sekou Toure.

“Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara kwenye eneo hilo lenye mwingiliano wa shughuli za kijamii. Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika ili afikishwe mahakamani,” imesema taarifa hiyo.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!