Latest Posts

NLD YAWATUPIA JICHO WANACHAMA ‘WALIOCHOSHWA’ CHADEMA

Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, ametumia fursa ya migogoro ndani ya CHADEMA kuwaalika rasmi wanachama wa kundi la G55 kujiunga na chama chake, akiwahakikishia jukwaa huru la kidemokrasia na fursa ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza hivi karibuni akiwa mkoani Tanga, Doyo amesema kuwa maelfu ya wanachama wa CHADEMA, akiwemo kundi la G55, wamekatishwa tamaa baada ya chama hicho kushindwa kusaini kanuni za uchaguzi, jambo linalowanyima haki yao ya kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.

“Siasa inafanyika popote pale. Ni suala la kujiamini,” amesema Doyo. “NLD ni daraja la matumaini kwa wote waliokosa jukwaa ndani ya vyama vyao. Tunawakaribisha G55 kujiunga nasi kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu.”

Msemaji wa kundi hilo, John Mrema, alisema kuwa wanachama hao walikuwa na dhamira ya kugombea nafasi mbalimbali, lakini wamevunjika moyo kutokana na kile walichokiita “kiburi cha viongozi wa chama chao ambao wameshindwa kusaini kanuni za uchaguzi.”

“Tulisubiria mchakato wa wazi na wa haki, lakini sasa tumebaki njia panda. Tumekuwa kama mayatima wa kisiasa,” alisema Mrema.

Akihitimisha, Doyo amesema kuwa chama chake ni jukwaa la matumaini mapya kwa Watanzania wote, na akaeleza kuwa alishawahi kutoka chama kingine na kujiunga na NLD kwa sababu ya imani ya kweli kwa mabadiliko.

“NLD ni daraja la demokrasia. Tunawaomba ndugu zetu G55 na wengine wenye dhamira njema wajiunge nasi. Tunahitaji wanasiasa wa kweli wenye lengo la kuwatumikia wananchi.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!