Latest Posts

RIPOTI YA UN YAISHUTUMU ISRAEL KWA UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU GAZA

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa (UN) wameishutumu Israel kwa kutumia unyanyasaji wa kingono na kijinsia dhidi ya Wapalestina na kutekeleza kile wanachokiita “vitendo vya mauaji ya halaiki” kupitia uharibifu wa vituo vya afya ya uzazi.

Ripoti hiyo, iliyoidhinishwa na Baraza la Haki za Kibinadamu la UN, inaripoti madai ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo ubakaji katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, baada ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, lililoanzisha vita kati ya Israel na Hamas.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa uharibifu wa hospitali za uzazi na uharibifu wa viinitete katika kliniki za uzazi unaweza kuwa mkakati wa kimakusudi wa kuzuia uzazi miongoni mwa kundi fulani, jambo ambalo linaweza kuangukia katika mojawapo ya vigezo vya mauaji ya halaiki kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Hata hivyo, Israel imekanusha vikali ripoti hiyo, ikiita madai hayo “yasiyo na msingi”. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameitaja ripoti hiyo kuwa ni shambulio la uongo dhidi ya Israel, akidai kuwa Baraza la Haki za Kibinadamu la UN ni taasisi inayopendelea Hamas na chuki dhidi ya Wayahudi.

Netanyahu amesema kuwa badala ya kushughulikia “uhalifu wa kivita unaofanywa na Hamas”, ripoti hiyo imeelekeza lawama kwa Israel kwa mashtaka ya uongo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!