Latest Posts

UTEKAJI BANDIA WA MTANDAONI WATESA WANAFUNZI WA KICHINA

Na Shabih Kassim.

 

Mtandao wa Al Jazeera kupitia kipindi cha 101 East umeripoti ongezeko la matapeli wa mtandaoni wanaotumia mbinu za kidigitali kuwalenga wanafunzi wa Kichina wanaosoma nje ya nchi kwa utapeli unaoitwa cyber kidnapping.

Katika aina hii ya utapeli, wanafunzi hulazimishwa kuigiza kuwa wametekwa nyara huku familia zao zikipokea picha na video za kutisha pamoja na madai ya kutuma fedha kama fidia.

Desemba 2023, mwanafunzi wa miaka 17, Kai Zhuang, aliripotiwa kutoweka Marekani. Familia yake ilitumiwa picha zake akiwa katika hali ya wasiwasi. Alipatikana siku chache baadaye akijificha kwenye milima ya Utah.

Miezi minne kabla, mwanafunzi mwingine wa kike mwenye umri wa miaka 22 alipotea nchini Australia, huku familia yake ikipokea picha zake akiwa amefungwa na kuonekana kama amejeruhiwa. Alikutwa akiwa salama ndani ya saa 24.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, wahalifu hutumia mbinu za hali ya juu kama udukuzi wa mawasiliano, ulaghai wa sauti na vitisho vya kisiasa kuwalazimisha wanafunzi kushiriki katika visa vya utekaji bandia kwa lengo la kupata pesa kutoka kwa familia zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!