Latest Posts

WAZAZI WAHIMIZWA KULINDA WATOTO DHIDI YA MATUKIO YA KIKATILI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara Abuu Athuman ameitaka jamii kuendelea kuwalinda watoto ili kupunguza matukio ya kikatili yanayo wakuta watoto hao.
Abuu amesema suala la kulinda watoto si jukumu la serikali pekee bali ni jukumu la kila mzazi na mlezi hivyo kila mtu anapaswa kuwa balozi wa kwa kuwalinda watoto hasa kubakwa na kulawitiwa.
Ameongeza kuwa utandawazi pia ni changamoto zinazopelekea watoto kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya,ulawiti na unyanyasaji mwengine wa kijinsia.
Mwenyekiti huyo ameyaeleza hayo kwenye mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana Nangwanda iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
Aidha kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM mkoa wa Mtwara Mohammed Abdallah maarufu Mudy Rey amechangia tofali 1000 na mifuko 30 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa uzio wa shule hiyo ya sekondari ya wasichana Nangwanda ili kuhakikisha wananfunzi hao wapata elimu kwenye mazingira salama zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!