Latest Posts

TAMISEMI YAAHIDI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

 

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) upande wa Afya, Dkt. Jafari Rajabu Seif, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma, kupeleka vifaa tiba vya kisasa na kuongeza wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye viwango.

Dkt. Seif ametoa kauli hiyo alipohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kilichofanyika katika Kata ya Nzera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika kuboresha sekta ya afya kwa kujenga na kukarabati hospitali, vituo vya afya na zahanati, sambamba na kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana na wataalamu wa afya wanaongezwa ili huduma ziwe karibu zaidi na wananchi.

“Azma ya serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya bila kujali anapoishi. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa tiba na kuongeza watumishi wa afya,” amesema Dkt. Seif.

Ameongeza kuwa maboresho yanayofanywa katika sekta ya afya yanalenga kupunguza changamoto zilizokuwepo kwa muda mrefu na kuongeza ubora wa huduma, hatua ambayo itaendelea kuleta tabasamu kwa wananchi na kuboresha ustawi wao.

Aidha, amewataka viongozi wa Chama na Serikali kuendelea kushirikiana katika kusimamia miradi ya maendeleo ili thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali ionekane kupitia huduma bora zinazowafikia wananchi.

Wananchi wa Wilaya ya Geita wameeleza kuwa maboresho yanayoendelea kufanywa na Serikali katika sekta ya afya yameongeza upatikanaji wa huduma muhimu, huku wakiiomba Serikali kuendelea kuwekeza zaidi ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la watu na kuimarisha huduma katika maeneo ya vijijini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!